Sunday, August 31, 2014

PHIRI APIGWA BUTWAA USAJILI WA OKWI


USAJILI wa straika Emmanuel Okwi ndani ya Simba, umemshtua kocha Patrick Phiri ambaye amesema haelewi nini kimetokea na sasa amewaachia viongozi waamue nani anafaa kuachwa ama kuendelea.
Juzi Alhamis jioni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe, alimtangaza rasmi Okwi kuwa mchezaji mpya wa Simba kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Mpaka jana Ijumaa mchana Okwi alikuwa hajajiunga na kambi hiyo iliyopo visiwani hapa huku kukiwepo taarifa kuwa angewasili muda wowote na taarifa za ndani zilisema kuwa beki Mkenya Donald Mosoti ndiye aliyekuwa kwenye mpango wa kuachwa.
Simba ilipitisha majina ya wachezaji 28 wakiwemo wachezaji watano wa kigeni ambao ni washambuliaji Amissi Tambwe, Raphael Kiongera, Pierre Kwizera, Joseph Owino na Mosoti.
“Bado nipo gizani, nimesikia taarifa hizo lakini nasubiri taarifa ya viongozi, naamini uongozi wa Simba upo vizuri katika kusajili hivyo mchezaji nitakayeletewa atakuwa mzuri maana wao wamemuona na amewahi kuichezea Simba,” alisema Phiri.
“Soka la Tanzania ni kama siasa hivyo tunatakiwa kukubaliana na hali halisi, mimi ni mtaalamu wa benchi la ufundi lakini viongozi pia wana utaalamu wao, hivyo naamini usajili wao utakuwa mzuri.”
Kuhusu taarifa za kutemwa kati ya wachezaji wake Mosoti au Tambwe, Phiri alisema: “Mosoti sikumpa nafasi sana ya kucheza mechi hizo kwa sababu wengi wanamfahamu na Butoyi Hussein amekuja kwa ajili ya majaribio hivyo ilikuwa ni lazima apewe nafasi ili aonyeshe kiwango chake.
“Tambwe ni mchezaji mzuri na ndiye mfungaji bora wa ligi msimu uliopita, binafsi alicheza vizuri pamoja na Said Ndemla katika mechi zilizopita, nikiwa kama kocha siwezi kusema mchezaji ameshuka kiwango kwa mechi za kirafiki.”

MUAFAKA WA KATIBA MPYA SASA WANUKIA


MKUTANO wa Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa juu wa vyama vya siasa uliofanyika jana mjini Dodoma umetajwa kuwa na dalili nzuri zinazoashiria mwafaka utapatikana juu ya mchakato wa utengenezaji
Katiba mpya. Kikwete alikutana jana na vyama hivyo kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachoongozwa na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo kukiwa na ajenda mbili mojawapo ikihusu mchakato unaoendelea wa kutengeneza Katiba mpya.
TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP. Ingawa
yaliyojiri ndani ya mkutano huo unaotajwa ulijaa amani na ucheshi hayakuwekwa wazi, Cheyo ambaye ni Mwenyekiti wa TCD alisema ajenda nyingine ilihusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Cheyo alisema mkutano huo ulienda vizuri na wamekubaliana Septemba 8, mwaka huu, kukutana kwa mazungumzo zaidi ambayo anaamini kutakuwa na matokeo chanya.
“Mkutano umeenda vizuri sana…ulikuwa mkutano mzuri sana, ulijaa amani na ucheshi. Tumekubaliana kwamba tunakutana tarehe 8, Septemba,” alisema Cheyo.
Akielezea imani yake juu ya mkutano huo wa wiki ijayo katika suala zima la kupata mwafaka juu ya mchakato wa Katiba mpya, baada ya Kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususa, Cheyo alisema, “…kukubaliana kukutana tu, ni jambo muhimu sana na lenye dalili nzuri.”
Kwa mujibu wa Cheyo, mkutano huo ulitawaliwa na utulivu, ucheshi jambo ambalo anaamini utamaduni wa Watanzania wa kukaa na kuzungumza utazaa matunda katika mkutano ujao.
Cheyo ambaye alishiriki pamoja na Katibu wa chama chake, Isack Cheyo, alisema wanachama wote wa TCD akiwemo mwakilishi wa vyama visivyo na wabunge, walihudhuria na kushiriki mkutano huo kwa ufasaha.
Kwa upande wa CCM, walioshiriki ni Makamu Mwenyekiti Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Chadema aliyeshiriki ni Katibu Mkuu wake, Dk Wilbrod Slaa pamoja na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu.
Washiriki wengine ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Katibu Mkuu wake, Mosena Nyambabe.
CUF iliwakilishwa na Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba na Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.
Kwa upande wa TLP, Mwenyekiti wake, Augustino Mrema na Katibu Mkuu wake, Jeremiah Shelukindo walishiriki.
Aidha Mwenyekiti wa United Peoples Democratic Party (UPDP), Fahmi Dovutwa aliwakilisha vyama visivyo na wabunge katika
TCD. Cheyo alisema kabla ya mkutano huo wa wiki ijayo, Septemba 6 na 7, TCD itakuwa na mkutano wake mkuu utakaokutanisha wanachama kabla ya kesho yake kukutana na Rais.
Ajenda kuhusu mchakato wa Katiba mpya, unazingatia hali ya sasa ya kisiasa ambayo, kundi la Ukawa lilisusa Bunge Maalumu la Katiba kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wake.
Tangu Ukawa wasuse Bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma, wananchi na makundi mbalimbali ya kijamii yamekuwa yakitaka wajumbe hao waliosusa warejee bungeni kuungana na wenzao waliobaki kutengeneza Katiba yenye maridhiano.
Licha ya kuwepo sauti za kusihi kundi hilo kurejea bungeni, pia wapo ambao wamekuwa wakisisitiza maridhiano kati ya Ukawana Tanzania Kwanza yapatikane ili kuunda Katiba yenye ushiriki wa makundi yote.
Wadau wengine, likiwemo Jukwaa la Wakristo Tanzania lililotoa taarifa yake jana kuhusu mchakato wa Katiba, na kumwomba
Rais Kikwete asitishe Bunge hilo ili upatikane mwafaka na maridhiano.Katika taarifa ya jukwaa hilo linalojumuisha Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Baraza la Makanisa ya Pentekoste (CPCT),
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Kanisa la Waadventista Wasabato, limeomba mchakato uahirishwe kuepusha athari kwa mshikamano na umoja wa taifa.
Mjadala bungeni kesho BUNGE Maalumu la Katiba litaanza majadiliano kesho baada kamati zote kumaliza kupitia na kuchambua sura zote za Rasimu ya Katiba. Jana na leo kwa mujibu wa Katibu wa Bunge hilo, Yahya Hamad kamati hizo ilikuwa ziwasilishe taarifa zao kwa Sekretarieti ya Bunge ambayo itaanza kuzichambua kabla ya kuzipeleka kwenye Bunge.
Hamad alisema licha ya kuzichambua, Kamati ya Uongozi itakutana leo kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali kabla ya majadiliano kuanza kesho.
"Ratiba yetu inaonesha kuwa Jumanne (kesho) Bunge lote litakutana kwa ajili ya majadiliano ambayo ni muhimu sana ili kuwekana sawa," alisema Hamad. Alisema siku 15 zimepangwa kwa ajili ya majadiliano ili taarifa hizo pamoja na maoni ya wajumbe wakati wa mjadala yawasilishwe kwa Kamati ya Uandishi wa Rasimu ya Katiba.
Hamad alisema Bunge hilo likishakamilisha mjadala, ndipo Kamati ya Uandishi wa Katiba ambayo iko chini ya Mwanasheria maarufu Andrew Chenge itaanza kazi ya kuandika Rasimu ya Katiba.
Alisema Kamati ya Chenge pia italazimika kurejesha Rasimu hiyo ndani ya Bunge kuona kile walichokiandika ni sahihi kabla ya kupigiwa kura na wajumbe wote. Bunge hilo limehitimisha siku 30 ambazo walizitumia kwa kamati mbalimbali kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba iliyowasilishwa bungeni hapo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Kwenye majadiliano hayo, kamati mbalimbali zilitupilia mbali baadhi ya mapendekezo yaliyoko kwenye Rasimu ya Katiba ikiwemo lile linalotaka wabunge wawe na ukomo na wananchi kupewa haki ya kumwondoa mbunge wao madarakani.
Eneo lingine ambalo baadhi ya kamati ziliyakataa ni ambayo yalitaka baadhi ya wateule wa Rais kutakiwa kuthibitishwa na Bunge kwa maelezo kuwa viongozi wanaotakiwa kuthibitishwa na chombo hicho, ni wale tu wanaowajibika kwa Bunge hilo.
Lakini pia kuna mvutano wa aina ya Bunge litakaloundwa kutokana na baadhi ya wajumbe kutaka mambo ya Tanzania Bara yajadiliwe na Watanzania Bara tu na pia yawepo mambo ya Muungano ambayo yatajadiliwa na wabunge kutoka pande zote za Muungano.

Hoja ya uraia pacha pamoja na suala la Kadhi Mkuu nalo ni miongoni mwa yanayodaiwa kukabiliwa na mvutano ndani ya baadhi ya kamati.
Source:Habari Leo

Saturday, August 30, 2014

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA MAMBO YA NJE


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/G/55 26 Agosti, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 31 kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua za maombi ya nafasi za kazi
kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu 2
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 September, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.3
1.0 AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II (SECOND SECRETARY) – NAFASI 10
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
1.1MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu masuala ya kimahusiano ya
kimataifa.
 Kuhudhuria mikutano mbalimbali.
 Kuandaa mahojiano.
 Kufuatilia masuala mbalimbali ya kimataifa.
 Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.
 Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali.
1.2SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa (B.A) ambao wamejiimarisha (major) katika
fani ya uhusiano wa Kimataifa (international Relations), Sheria au Uchumi kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
Aidha, wawe wamefanya na kufaulu mtihani unaotolewa Chuo cha Diplomasia,
Dar es Salaam.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
2.0 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III) –
NAFASI 11
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
 Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa.
 Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao,
safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
 Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote
kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
 Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia
kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
 Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na
kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
 Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.4
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu
mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na
Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya
Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti
katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
2.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
3.0 AFISA UTUMISHI DARAJA LA II (HUMAN RESOURCES OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutunza Kumbukumbu sahihi za watumishi wote katika Wizara, Mikoa, Wilaya na
Idara zinazojitegemea kulingana na mahali alipo.
 Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi.
 Kutafiti, kuchanganua na kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
 Kuandaa na kupanga mipango ya mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
 Kukadiria na kupanga mahitaji ya vifaa vya mafunzo kwa kushirikiana na vyuo
vilivyopo chini ya sekta zinazohusika.
 Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu
mipango ya watumishi.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi Jamii au Sanaa kutoka katika
Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao wamejiimarisha (major) katika
mojawapo ya fani zifuatazo:-
 Menejimenti ya Raslimali Watu (Human Resources Management).
 Elimu ya Jamii (Sociologly).
 Utawala na Uongozi (Public Administration).
 Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.5
4.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
 Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia
ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
 Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
 Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
 Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
 Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au
wamepata idhni ya maafisa husika.
 Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
 Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
 Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa
kwenda nje.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili
na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
4.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
5.0 MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia,
kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji
bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
 Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofsa waoaohusika na
kuyarudisha sehemu zinazohusika.
 Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
 Kutayarisha chai ya ofisi.
 Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
 Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
 Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga
baada ya Saa za Kazi.6
 Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
 Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
 Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya
Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
5.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
 X.M. DAUDI
 Katibu
 Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Tembelea  hapa  kwa maelezo zaidi

ILRI Consultancy: IT Specialist | Jobs In East Africa

Changamkia nafasi za ajira hapo chini

ILRI Consultancy: IT Specialist | Jobs In East Africa


MAGAZETI YA LEO HAPA

1_18e8e.jpg
2_83c18.jpg
3_46971.jpg
4_f0ce7.jpg
10_c2ce7.jpg
11_d4d16.jpg
13_c9a98.jpg

BARUA ZA YANGA KUOMBA MKATABA WA OKWI NA SIMBA UVUNJWE HIZI HAPA


Ukurasa wa kwanza wa barua waliyoandika yanga kutaka mkataba wa okwi na simba uvunjwe.chini ni Ukurasa wa pili wa barua hiyo...

Na Hii hapo chini ni barua TFF kuwaita pamoja..

TORRES NAYE SASA ATIMKA CHELSEA

IMG_6865.JPG
Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo.
Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kwa ada ya uhamisho ambayo ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza – £50m akitokea Liverpool – leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo sasa anajiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili.
Torres anajiunga na AC Milan kwenda kurithi nafasi ya Mario Balotelli ambaye amejiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa £16m.
Torres ameichezea Chelsea mechi 172 na kufanikiwa kuifungia magoli 45 tangu alipotia mguu Stamford Bridge.
Mchezaji huyo anategemewa kwenda kuchezea klabu ya AC Milan  katika msimu huu.

Friday, August 29, 2014

MWALIMU ABAKWA NA MWINGINE KUPORWA 20 MILIONI

                                          Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi
Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamemteka na kumvamia mwalimu mmoja na kumpora kiasi cha zaidi ya Sh milioni 20 na kisha kumbaka mwalimu mwingine wa kike katika kijiji cha Nassa Ginery wilayani Busega mkoani Simiyu.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Simiyu, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi kijijini hapo.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Simiyu, Evance Mwijage ndiye aliyethibitisha kuwapo kwa tukio hilo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu.
Hata hivyo, hakuwa tayari kuelezea zaidi taarifa juu ya tukio hilo, akisema alikuwa anasubiri jalada la Polisi kutoka wilayani Busega ambalo lina taarifa za kina, ikiwa ni pamoja na watu wanaohusishwa na tukio zima.
Lakini kwa upande wa mwalimu aliyetekwa na kuporwa fedha, Samwel Mbochi alisema siku ya tukio, watu anaoamini kuwa ni majambazi waliruka ukuta wa nyumba yake na kumvamia na kumshikilia wakimtaka atoe pesa.
Anasema alitii amri yao na kutoa kiasi hicho cha fedha alichokuwa amekiandaa kwa ajili ya kununua bidhaa kesho yake, kwani pamoja na kuwa mwalimu, pia amekuwa akijishughulisha na biashara ya duka kijijini hapo.

Anaongeza kuwa, baada ya kuchukua fedha, walivamia chumba kingine cha mwalimu wa kike ambaye ni mpangaji wake na kumbaka kwa zamu, kisha kutokomea kusikojulikana.

XABI KUTIMKIA BAYERN, KWA ANCHELLOTI SASA PAMEJAA.

Mabingwa Bundesliga Bayern Munich wametangaza kukubaliana na mabigwawa Ulaya klabu ya Real Madrid juu ya uhamisho wa Kiungo mkongwe Xabi Alonso, kuziba nafasi za majeruhi zilizo wachwa na Javi Martinez, Bastian Shwanstiger na Thiago Alcantara.
Bayern Munich have made a move for Xabi Alonso
Akithibitisha mbele ya waandishiwa Habari, mkurugenzi wa bodi ya Bayern munich, Jan-ChristianJeseen,  amesema kuwa klabu hizo zimekubaliana kuhusu uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wamika 32 na anafanyiwa vipimo vya afya leo Agosti 28, 2014. 

Alonso alijiungana Real Madrid mwaka 2009, akitokea Liverpool na kufanikiwa kuichezea m
Madrid mechi zaidi ya 200, mkataba wa awali wa Alonso ulikuwa unamalizika mwaka 2016, lakini analazimika kuondoka Santiago Bernabeukutokana na ugumu wanafasi katika kikosi cha kwanza cha Carlo Anchelloti kutokana na uwepo wa Toni Kroos aliye jiunga naklabu hiyo akitokea Bayern Munich Julai mwakahuu.


Thursday, August 28, 2014

OKWI ATUA TENA SIMBA, ASAINI MIAKA MIWILI


Pichani ni Emmanuel Okwi

Yametimia, hatimaye Emmanuel Okwi amerejea katika kikosi chake cha zamani cha Simba.
Okwi rasmi anasaini leo kujiunga na Simba baada ya kuelewana na uongozi wa klabu hiyo.
Mganda huyo amechukua uamuzi wa kusaini kuichezea Simba baada ya Yanga kumtema.


MKURUGENZI WA TBS AFUNGWA MIAKA 3 JELA


Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu DSM, imemhukumu kwenda jela miaka 3 aliyekuwa mkurugenzi wa TBS Bwana Charles Ikerege baada ya kukutwa na hatia katika makosa yaliyokuwa yakimkabili, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

Tuesday, August 26, 2014

RONALDO KUTUA RASMI TANZANIA

BAADA ya kuwaona magwiji wa Real Madrid wakiongozwa na Luis Figo, sasa mashabiki wa soka wa Tanzania watakishuhudia kikosi cha sasa cha timu hiyo bingwa wa bara la Ulaya.

 Juzi Jumamosi, Figo akiwa na mwanasoka mwingine mahiri wa zamani duniani, Fabio Cannavaro, walicheza kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mbele ya maelfu ya mashabiki. Katika pambano hilo la kimataifa la kirafiki dhidi ya kikosi cha wakongwe nchini, Tanzania XI, Real Madrid walishinda mabao 3-1.
Baada ya kuvutiwa na mchezo huo uliowagusa maelfu ya Watanzania ambao uliratibiwa na Kampuni ya TSN Supermarkets, Real Madrid ya sasa inaletwa nchini kama magwiji hao.
Rais Jakaya Kikwete aliyeshuhudia pambano hilo akitokea safarini kikazi mikoa ya Morogoro na Arusha, ameweka wazi kuwa mipango ya kuwaleta kina Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, James Rodriguez na wengine imeanza.
“Watanzania wamefurahishwa sana na kuja kwenu pamoja na pambano safi walililoona jioni ya leo (juzi) pale uwanjani.
“Sasa tunataka ije timu ya sasa ya Real Madrid. Nimezungumza na Balozi (wa Hispania nchini), atasimamia jukumu hilo,” alisema Rais Kikwete, juzi usiku Ikulu katika chakula cha usiku alichokiandaa kwa timu hizo mbili.
Balozi wa Hispania nchini, Luis Manuel Civis, alikuwa miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.
Rais Kikwete ambaye chini ya utawala wake, amekuwa mstari wa mbele kusaidia sekta ya michezo, alisema mashabiki wa soka na Watanzania kwa ujumla waliojitokeza Taifa, wamefurahishwa sana na pambano hilo la juzi.
Aidha, Rais Kikwete alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Real Madrid utaendelezwa zaidi kwa kuhakikisha miamba hiyo inajenga kituo chake cha mafunzo ya soka kwa vijana.
Magwiji hao wa zamani mbali ya kupata fursa ya kula chakula na Rais Kikwete na viongozi wengine wa Serikali, pia Rais aliwapa kila mmoja zawadi ya kinyago cha Kimakonde.</p>
Awali, Figo na wenzake akiwamo nahodha wa Italia aliyetwaa Kombe la Dunia 2006, Fabio Cannavaro walimkabidhi Rais jezi iliyosainiwa na wachezaji wa timu hiyo bingwa wa Ulaya.
Aidha, wachezaji hao walimpatia pia jezi kama hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TSN Supermarkets, Farough Baghozah, ambaye amefanikisha ziara hiyo ya kwanza ya aina yake kwa miamba hiyo Tanzania na barani Afrika.

Magwiji hao wa Real Madrid jana walitarajiwa kutembelea mlima Kilimanjaro mjini Moshi na leo watakuwa Arusha kutembelea kreta ya Ngorongoro kabla ya kurejea makwao kesho.

EBOLA SASA TISHIO DRC,NCHI JIRANI IKIWEMO TANZANIA ZAHADHARISHWA.

SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imebaini kuwepo kwa mlipuko wa maradhi ya homa kali maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo, ambayo sasa imethibitika kuwa ni ugonjwa wa ebola.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Dk Felix Numbi, aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana, kwamba watu wawili wamepimwa na kugundulika wanaumwa ebola, maradhi ambayo hadi sasa yameshaua watu 13 katika jimbo la Equateur.
Lakini, maradhi hayo yako maeneo ya vijijini na imeelezwa kuwa ebola hiyo, ni tofauti na ile inayosumbua nchi za Afrika Magharibi. Shirika la Afya Duniani (WHO) limekiri kuwa mlipuko wa ebola kwa sasa hautarajiwi kuwa na kasi kubwa katika nchi za Afrika Magharibi, ambako tayari watu 2,615 wameshakumbwa na maradhi hayo tangu ulipuke Machi mwaka huu.
Hadi sasa maradhi hayo hayana tiba, lakini baadhi ya wagonjwa wamepona baada ya kupewa dawa aina ya ZMapp, ambayo bado iko kwenye majaribio.
Hata hivyo, dawa hizo zimemalizika na hazipo tena. Dk Numbi alisema watatangaza karantini ya watu kuingia na kutoka katika mji wa Boende, ambako wagonjwa wa homa hiyo wamegundulika.
 Mji huo upo kilometa 100 kutoka jiji la Kinshasa. Alisema kuibuka tena kwa mlipuko huo, kumesababisha idadi ya milipuko ya homa ya ebola kufikia saba tangu 1976 mgonjwa wa kwanza alipogundulika karibu na Mto Ebola.
Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu tishio la ugonjwa huo katika nchi jirani na Tanzania, Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anayeshughulikia Dharura na Maafa, Dk Elias Kwesi, alisema Serikali imeendelea kuimarisha ulinzi na usalama mipakani na katika viwanja vya ndege.
 Dk Kwesi alisema ulinzi huo, umeenda sambamba na upimaji wa afya za watu wanaoingia nchini, ili kukabiliana na ugonjwa huo. Alisema mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka WHO za kuwepo kwa ugonjwa huo nchini Kongo.
 Dk Kwesi alisema mpaka sasa tayari wameshafunga vifaa vya kisasa katika viwanja vyote vya ndege.
Mpango uliopo ni kufunga vifaa vingine katika mipaka yote na tayari utekelezaji wa mpango huo, umeshaanza katika mpaka wa Namanga.
Kwa mujibu wa Dk Kwesi, wiki hii wanatarajia vifaa vingine vya upimaji kuwasili na vitasambazwa katika mipaka ya Holili, Sirari na Mtukula.
Lengo ni kuhakikisha mipaka yote imefungwa vifaa hivyo, ili watu wanaoingia kupitia mipaka hiyo, wapimwe afya zao kwanza.
 Alisema tayari wameshatoa mafunzo kwa wataalamu wa afya wa mikoa mbalimbali, ikiwemo mikoa ya pembezoni ambayo nao wanatakiwa kufundisha wahudumu wa afya na jamii dalili za ugonjwa huo na namna ya kukabiliana nao. Dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa na vidonda kooni.
Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini. Muda wa kuonekana kwa dalili za ugonjwa huo ni kati ya siku mbili hadi 21 baada ya kupata maambukizi.
“Ugonjwa wa ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo, kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huo na kugusa wanyama walioambukizwa mizoga na wazima kama vile sokwe na swala wa msituni,” imeeleza taarifa ya Wizara ya Afya iliyotolewa hivi karibuni.
Katika hatua nyingine, baada ya ugonjwa huo kuua madaktari na wataalamu wa maabara, Taasisi ya Kupambana na Magonjwa Ambukizi Kusini mwa Jangwa la Sahara (SACIDS), imeamua kutoa mafunzo kwa wataalamu hao, ili kusaidia waepukane na hatari ya kuambukizwa magonjwa hayo.
Wataalamu na wanafunzi hao 45 kutoka katika ukanda huo, ikiwemo, Kenya, Uganda, Kongo DRC, Zambia, Msumbiji, Afrika Kusini na mwenyeji Tanzania, walikutana mkoani Morogoro kujadili umuhimu wa kuongeza usalama katika kuhifadhi sampuli za ugonjwa huo ili zisisambae.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Profesa Mark Rweyemamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), alisema wameamua kuchukua wataalamu na wanafunzi kutoka katika nchi hizo, ili wapate elimu ya jinsi ya kujikinga, ikiwa kutatokea mlipuko wowote wa ugonjwa huo.
Alisema kuwa asilimia 20 ya watu katoka katika ukanda huo, hufariki dunia kwa magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa bindamu.
Mhadhiri wa SUA, Esron Karimuribo, alisema Bara la Afrika limekuwa likikumbwa na magonjwa mengi ambukizi, ikiwemo ebola na magonjwa mengine yanayofanana na hayo.
Alisema kuwa ushirikiano kati ya sekta ya afya na mifugo, ni muhimu kwa kuwa magonjwa mengi yanayowapata binadamu yanatokana na mifugo.
Mkuu wa Idara ya Maikrobayolojia na Parasitolijia katika Kitivo cha Mifugo cha SUA, Gerald Misinzo, alitoa mfano wa homa ya bonde la ufa, kuwa huathiri wanyama na binadamu.
Mkurugenzi wa Sayansi ya Uhai Tanzania, Flora Ismail, alisema bioteknolojia inatoa suluhu kinzani za magonjwa, ikiwa ni pamoja na kuzalisha chanjo ya magonjwa mbali mbali yanayosababishwa na wanyama na katika kilimo wamepata suluhu kwa kuchagua mbegu bora.

Imeandikwa na Shadrack Sagati, Hellen Mlacky, Dar, Agnes Haule, Morogoro na mashirika ya habari.
Source:Habari Leo

Friday, August 22, 2014

MANCHESTER UNITED YAPAMBANA 'KUFA KUPONA' KUWANASA DI MARIA, SAMI KHEDIRA

Pair of aces: Angel Di Maria (left) and Sami Khedira are both on Manchester United's radar
Wote kwenye rada: Angel Di Maria (kushoto) na Sami Khedira wanatakiwa na Manchester United.
MANCHESTER United bado wanapambana kuhakikisha wanawasajili nyota wawili wa Real Madrid, Muargentina, Angel di Maria na Mjerumani Sami Khedira.
Habari njema kwa mashabiki wa United ni kwamba makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward anapigana kuwasajili wachezaji hao kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema jumanne kuwa Di Maria na Khedira wanaweza kuondoka.
Di Maria amekuwa katika rada za Louis Van Gaal kwa majira yote ya kiangazi wakati Khedira alimuona wakati anafundisha soka nchini Ujerumani.
Wanted: Di Maria remains a top target for Louis van Gaal and Manchester United this summer
Di Maria ndiye chaguo namaba moja la Luis Van Gaal na Manchester United majira haya ya kiangazi.
Open offer: Carlo Ancelotti says ¿if Di Maria doesn¿t find a solution for his future, we would welcome him back'
Milango iko wazi: Naye meneja wa Real madrid Carlo ancelott amesema, "Kama Di Maria hatapata hatima yake ya baadae, kwa furaha tunamkaribisha tena "

HII NDIO KAULI YA EMMANUEL OKWI KUHUSU YANGA SC


‘Mimi na Yanga tulikua na makubaliano ya mkataba na hakuna ukweli kwamba Mshahara niliokua nalipwa Yanga ni mdogo, mshahara usingekua unatosha nisingekubali kusaini mkataba‘
‘Ni kweli kuna mambo mengi hayapo sawa kati yangu na club yangu yaYanga ila ni mambo ya ndani ambayo nisingependa kuyazungumzia, ni mambo madogo ambayo nadhani yanaweza kuisha‘
‘Hakuna ukweli kwamba mimi nakwenda Ulaya, sijui hata imetoka wapi na nani kaanzisha hii ya Ulaya, mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga na huwa naongea nao karibu kila siku, hata jana nimetoka kuongea na katibu mkuu na mambo yote yanaelekea vizuri hamna shida yoyote mpaka sasa hivi‘ - Hii ni kauli ya mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Anord Okwi.

Wednesday, August 20, 2014

LUIS FIGO KUONGOZA MSAFARA WA KWANZA WA MAGWIJI WA REAL MADRID KUTUA NCHINI KESHO


MSAFARA wa kwanza wa magwiji wa Real Madrid, ‘Real Madrid Legends’ utatua nchini Tanzania kesho, ukitarajiwa kuongozwa na mwanasoka bora wa zamani wa dunia na Ulaya, Mreno, Luis Filipe Madeira Figo.
Magwiji hao watashuka dimbani jumamosi Agosti 23 dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa zamani wa Tanzania ‘Tanzania All Stars’ ndani ya uwanja wa kisasa wa Taifa, jijini Dar es salaam.
Figo ataongozana na nyota wengine wawili waliotamba na Real Madrid miaka ya nyuma, Muingereza Michael Owen na Christian Karembeu.
Figo aliyestaafu soka mwaka 2009, alishinda tuzo mbili mfululizo mwaka 2000 ambazo mwanasoka bora wa Ulya na Dunia na katika enzi zake za kucheza soka alikuwa mchezaji hatari kupita maelezo na sasa anakuja kukumbushia ufundi wake katika ardhi ya Rais Jakaya Kikwete.
Mbali na Figo, mwanasoka mwingine bora wa zamani wa dunia, Zinedine Zidane na Mbrazil Ronaldo de Lima wanatarajia kutua nchini Ijumaa na kundi kubwa la magwiji hao.

Mkurugenzi wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN) (waandaaji wa ziara hiyo), Farough Baghozah amekaririwa akisema mapokezi makubwa kwa ajili ya magwiji hao yameandaliwa na watawasili kwa mafungu, lakini kundi kubwa litaingia nchini Agosti 22.

Baghozah alisema magwiji hao watapokelewa kwa maandamano kutoka uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam na kupelekwa hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach.
 Tayari kikosi cha ‘Tanzania All Stars’ kimeanza mazoezi katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam chini ya kocha maarufu, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’akisaidiwa na Fredy Felix Minziro na Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’.
Mlinda mlango na nahodha wa kikosi hicho, Mohamed Mwamweja ametoa wito wa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwaona nyota wao wa zamani kwasababu wamejipanga vizuri.
 Mwamweja alikiri kuwa wamekaa muda mrefu bila kucheza mpira, lakini mazoezi hayo yamewaongezea nguvu ya kucheza mechi hiyo.
Kipa huyo anayetarajia kuanza katika kikosi cha kwanza alisema watajifunza mengi kutoka kwa magwiji hao, lakini nao watajifunza vitu fulani kutoka kwa wachezaji wa Tanzania.
Wachezaji wanaoendelea kujifua kwa ajili ya kukumbushia enzi zao na magwiji wa Real Madrid ni:
Makipa waliowahi kutamba nchini Tanzania, Mohamed Mwameja na Peter Manyika.
Watakaosuka safu ya ulinzi ni mabeki Shadrack John Nsajigwa Mwandemele, Boniface Pawasa, John Mwansasu,  Mecky Mexime, Abubakar Kombo, George Masatu na Habib Kondo, 
Viungo ni:  Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho Musso, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.

Washambuliaji: Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel Mwakyusa, Said Maulid ‘SMG’, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, 
Madaraka Suleiman ‘Mzee wa Kiminyio’ na Akida Makunda.

KIKOSI CHA AZAM FC KINACHOANZA LEO DHIDI YA EL MERREIKH-ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME


Leo tarehe 20.08.2014 timu ya Azam FC itaingia Uwanjani kupambana na El merreikh ya Sudan katika mchezo wa robo fainali ya CECAFA KAGAME CUP. Mchezo utaanza saa 8:30 mchana kwa saa za Rwanda na itakua sa9:30 Dar.
Wawakilishi wa leo ni;
1 . MWADINI ALI
2. SHOMARI KAPOMBE
3. ERASTO NYONI
4. DAVID MWANTIKA
5. AGGREY MORIS
6. BOLOU MICHAEL
7. HIMIDI MAO
8. SALUM ABUBAKAR
9. JOHN BOCCO
10 KIPRE TCHETCHE
11. LEONEL SAINT PREUX
AKIBA
AISHI MANULA
MUDATHIR YAHYA
SAID MORAD
DIDIER KAVUMBAGU
GAUDENCE MWAIKIMBA
GADIEL MICHAEL
KHAMISI MCHA

Friday, August 15, 2014

Wasukuma sasa marufuku kutembea na fimbo mtaani,Ngoma za Chagula Mayu nazo zapigwa marufuku!


UONGOZI wa Serikali kwenye Tarafa ya Ngaherango, Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, umepiga marufuku wafugaji wa kabila la Wasukuma kwenye tarafa hiyo, kutembea na fimbo mitaani ili kukomesha tabia ya kuchapana ovyo hata kusababisha mauaji.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye vijiji vya Ngoheranga na Ihowanja wilayani humo, Ofisa Tarafa wa Kijiji cha Ngoheranga, Conrad Mzwalandili, alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na malalamiko ya wananchi juu ya matumizi mabaya ya fimbo hizo.
Katika mkutano huo, wananchi walitaka kujua sababu za uongozi wa Serikali katika tarafa hiyo kutoa agizo hilo wakati wafugaji wa kabila hilo ni utamaduni wao kutembea na fimbo.
Mzwalandili alisema, imebainika baadhi ya vijana ambao hutembea na fimbo, huchapana hata kusababisha mauaji na tayari zaidi ya fimbo sabini zimekamatwa akiwataka wakazi wa eneo hilo kutembea kwa kujiamini kwani Tanzania ni nchi huru.
Mbali ya agizo hilo, pia alisema wamepiga marufuku ngoma aina ya chagulaga ambayo imekuwa ikiwadhalilisha mabinti wakiwemo wanafunzi ambapo vijana zaidi ya 100, humkimbiza binti bila kujali ni mwanafunzi au vinginevyo na kumfanyia vitendo visivyofaa.
Kama ni tamaduni zenu, fanyieni nyumbani kwenu tena ndani na si barabarani...yeyote ambaye atakwenda kinyume na agizo hili atachukuliwa hatua,alisema Mzwalandili na kusisitiza Kamati ya Ulinzi na Usalama imeridhia kupigwa marufuku ngoma hiyo, kutembea na fimbo.

Thursday, August 14, 2014

Diamond ashinda Tena Tuzo ya TTTMAwards nchini Burundi

Soma hapo chini alichokiandika Instagram baada ya kushinda Tuzo hiyo


MKE WA KIGOGO APIGWA RISASI KWAPANI MKOANI ARUSHA

Jeraha la mgongoni alilopata Flora Porokwa.

MKE wa Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wafugaji la Pingos Forum, Edward Porokwa, Flora Porokwa (37), mkazi wa Sakina Kwaidi amepigwa risasi na watu wanaohisiwa kuwa ni majambazi.

Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo risasi hiyo alipigwa kwapani na kwenda kutokea mgongoni na kulazimika kuendesha gari umbali wa kilometa moja akiwa na risasi mwilini.

Majeruhi huyo ambaye  amelazwa katika Hospitali ya Seliani jijini hapa, alionesha ujasiri wa hali ya juu baada ya kumudu kuendesha gari hilo huku watu hao wawili waliokuwa wamepanda bodaboda wakiendelea kumfuatilia hadi alipofika nje ya nyumba yake ambapo aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu akiwa anasubiri kufunguliwa geti la kuingia ndani.

Akizungumza kwa tabu hospitalini hapo, majeruhi huyo alisema tukio hilo lilimtokea jioni ya saa moja kasoro katika Barabara ya Arusha - Namanga eneo la Kwaidi ambapo watu hao walimvamia ghafla na kulizuia gari lake kwa mbele wakitumia  pikipiki hiyo.

Alisema mmoja wa watu hao alimfuata na kushika kitasa cha mlango wa mbele na kujaribu kufungua lakini mlango haukufunguka. Ndipo mwanamke huyo alipoamua kushusha kioo cha mlango ili aweze kumsikiliza, lakini ghafla jambazi huyo alichomoa bastola na kumpiga risasi kwapani.

“Kwenye gari sikuwa na fedha, sijui kama walilenga kunipora au kuna tatizo lingine. Nikiwaona naweza kuwakumbuka kwa sura ila siwajui, sikuwahi kuwaona kabla,’’ alisema mwanamke huyo na kuongeza kuwa:

“Namshukuru Mungu kwa kuniepusha na kifo kwani dhamira yao ilikuwa kuniua.”

Majeruhi huyo ambaye hali yake bado siyo vizuri, alitoa rai kwa jeshi la polisi mkoani Arusha kuwasaka watu hao kisha kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Hadi sasa tukio hilo halijafahamika undani wake kama watu hao walilenga kupora fedha au ni  kisasi, kwani kabla ya tukio hilo kuna taarifa kwamba hata mumewe, Porokwa aliwahi kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Jirani mmoja wa mama huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema wamesikitishwa mno na tukio la mwenzao kupigwa risasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.