Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi
Watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi wamemteka na kumvamia mwalimu mmoja na kumpora
kiasi cha zaidi ya Sh milioni 20 na kisha kumbaka mwalimu mwingine wa kike
katika kijiji cha Nassa Ginery wilayani Busega mkoani Simiyu.
Kwa
mujibu wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Simiyu, tukio hilo lilitokea usiku wa
kuamkia juzi kijijini hapo.
Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Simiyu, Evance Mwijage ndiye
aliyethibitisha kuwapo kwa tukio hilo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi
kwa njia ya simu.
Hata
hivyo, hakuwa tayari kuelezea zaidi taarifa juu ya tukio hilo, akisema alikuwa
anasubiri jalada la Polisi kutoka wilayani Busega ambalo lina taarifa za kina,
ikiwa ni pamoja na watu wanaohusishwa na tukio zima.
Lakini
kwa upande wa mwalimu aliyetekwa na kuporwa fedha, Samwel Mbochi alisema siku
ya tukio, watu anaoamini kuwa ni majambazi waliruka ukuta wa nyumba yake na
kumvamia na kumshikilia wakimtaka atoe pesa.
Anasema
alitii amri yao na kutoa kiasi hicho cha fedha alichokuwa amekiandaa kwa ajili
ya kununua bidhaa kesho yake, kwani pamoja na kuwa mwalimu, pia amekuwa
akijishughulisha na biashara ya duka kijijini hapo.
Anaongeza
kuwa, baada ya kuchukua fedha, walivamia chumba kingine cha mwalimu wa kike
ambaye ni mpangaji wake na kumbaka kwa zamu, kisha kutokomea kusikojulikana.

No comments:
Post a Comment