Wote kwenye rada: Angel Di Maria (kushoto) na Sami Khedira wanatakiwa na Manchester United.
MANCHESTER
United bado wanapambana kuhakikisha wanawasajili nyota wawili wa Real Madrid,
Muargentina, Angel di Maria na Mjerumani Sami Khedira.
Habari
njema kwa mashabiki wa United ni kwamba makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed
Woodward anapigana kuwasajili wachezaji hao kabla ya kufungwa kwa dirisha la
usajili.
Kocha
wa Real Madrid, Carlo Ancelotti alisema jumanne kuwa Di Maria na Khedira
wanaweza kuondoka.
Di
Maria amekuwa katika rada za Louis Van Gaal kwa majira yote ya kiangazi wakati
Khedira alimuona wakati anafundisha soka nchini Ujerumani.
Di Maria ndiye chaguo namaba moja la Luis Van Gaal na Manchester United majira haya ya kiangazi.

Milango iko wazi: Naye meneja wa Real madrid Carlo ancelott amesema, "Kama Di Maria hatapata hatima yake ya baadae, kwa furaha tunamkaribisha tena "
No comments:
Post a Comment