
UONGOZI wa Serikali kwenye Tarafa ya Ngaherango, Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro, umepiga marufuku wafugaji wa kabila la Wasukuma kwenye tarafa hiyo, kutembea na fimbo mitaani ili kukomesha tabia ya kuchapana ovyo hata kusababisha mauaji.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara kwenye vijiji vya Ngoheranga na Ihowanja wilayani
humo, Ofisa Tarafa wa Kijiji cha Ngoheranga, Conrad Mzwalandili, alisema
wamefikia hatua hiyo kutokana na malalamiko ya wananchi juu ya matumizi mabaya
ya fimbo hizo.
Katika
mkutano huo, wananchi walitaka kujua sababu za uongozi wa Serikali katika
tarafa hiyo kutoa agizo hilo wakati wafugaji wa kabila hilo ni utamaduni wao
kutembea na fimbo.
Mzwalandili
alisema, imebainika baadhi ya vijana ambao hutembea na fimbo, huchapana hata
kusababisha mauaji na tayari zaidi ya fimbo sabini zimekamatwa akiwataka wakazi
wa eneo hilo kutembea kwa kujiamini kwani Tanzania ni nchi huru.
Mbali
ya agizo hilo, pia alisema wamepiga marufuku ngoma aina ya chagulaga ambayo
imekuwa ikiwadhalilisha mabinti wakiwemo wanafunzi ambapo vijana zaidi ya 100,
humkimbiza binti bila kujali ni mwanafunzi au vinginevyo na kumfanyia vitendo
visivyofaa.
Kama
ni tamaduni zenu, fanyieni nyumbani kwenu tena ndani na si barabarani...yeyote
ambaye atakwenda kinyume na agizo hili atachukuliwa hatua,alisema Mzwalandili
na kusisitiza Kamati ya Ulinzi na Usalama imeridhia kupigwa marufuku ngoma
hiyo, kutembea na fimbo.
No comments:
Post a Comment