Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Friday, September 5, 2014

Aliyempiga kichwa mwamuzi aadhibiwa



  
                                              Ismail Gunduz
Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kuto cheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani mwamuzi wa mchezo.
Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.
Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.

Wednesday, September 3, 2014

VAN PERSIE:NIKO TAYARI KUPIGANIA NAMBA NA FALCAO

Van Persie: I'm ready to fight Falcao
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie amesema yuko tayari kupigania namba na mchezaji mwenzake Radamel Falcao katika klabu ya Manchester United. Baada ya usajili wa Falcao sasakuna wachezaji kadhaa watakaopigania namba katika klabu hiyo.
Wachezaji watakopigania namba katika klabu hiyo ni Wayne Rooney, Van Persie and Juan Mata.

Tuesday, September 2, 2014

HUU NDIO UHAMISHO WA WACHEZAJI KUMI GHALI ZAIDI KUFANYIKA KWENYE DIRISHA HILI LA USAJIRI.

Suarez to Barcelona and the 10 most expensive transfers of the summer
Dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi kwa vilabu majira haya ya kiangazi limefungwa hapo jana usiku tukishuhudia miezi kadhaa ya kufuru ya matumizi yaliyokithili ya pesa kwa vilabu barani Ulaya.

Japokuwa rekodi ya uhamisho ghali zaidi duniani inashikiriwa na Gareth Bale ya uhamisho wa Euro milioni 100 alipohama kutoka Tottenham kwenda Real Madrid mwaka uliopita lakini mado suala la matumizi ya fedha na uvunjwaji wa rekodi mbalimbali linabakia palepale kwa vilabu kadhaa barani Ulaya.
Little bit hefty! United paid a club record £60million for Real Madrid midfielder Angel di Maria 
Wakati vilabu vikiendelea kusharehekea mapato makubwa kwenye matangazo na mauzo ya vifaa mbalimbali isivyo kawaida na vikienda kwenye duka kuu la ununuzi wa wachezaji ambalo ni michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika kule nchini Brazil, Vilabu vinaonekana kuongeza ushindani pia kwenye matumizi ya mapato hayo makubwa wanayojikusanyia kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.

Ufuatao ni usajili wa wachezaji kumi ambao wamenunuliwa kwa mahela mengi kwenye msimu huu wa manunuzi.
No.MchezajiKutokaKwendaAda (Euro)
1Luis SuarezLiverpoolBarcelona88m
2James RodriguezMonacoReal Madrid80m
3Angel Di MariaReal MadridManchester United75m
4David LuizChelseaParis Saint-Germain49.5m
5Eliaquim MangalaPortoManchester City44.5m
6Diego CostaAtletico MadridChelsea44m
7Alexis SanchezBarcelonaArsenal40m
8Luke ShawSouthamptonManchester United37.8m
9Ander HerreraAthletic BilbaoManchester United36.5m
10Cesc FabregasBarcelonaChelsea36m

Monday, September 1, 2014

Dirisha la Usajili lafungwa Rasmi

Baadhi ya wachezaji kwenye kikosi cha man united
Dirisha la kimataifa la usajili limefungwa jana huku Manchester united wakiibuka kidedea.
Man United imevipiku vilabu vingine vya soka baada ya kumnyakua mshambulia nguli Radamel Falcao kutoka klabu ya Monaco kwa kiasi cha pound milioni 6 huo ukiwa ni mkopo wa muda mrefu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akiwa na klabu ya Monaco hadi anafungasha virago na kuondoka ameifungia Monaco ya Ufaransa jumla ya mabao 11 katika mechi 20.

Nao Arsenal wamemchukua mshambuliaji wa Man United Danny Welbeck kwa mkopo wa pound million 16. Matumaini ni makubwa kwa mshambuliaji huyo anayetua katika uwanja wa Emirates huku mashabiki wake wakionyesha Imani kubwa kwake katika msimu huu.


MAN UNITED KUNASA SAINI YA FALCAO


Leo ni siku ya mwisho ya kusajili wachezaji wapya katika vilabu vya soka nchini Uingereza.
Klabu ya Manchester United ndio inalenga kuweka kufuli kwenye dirisha la usajili wa wachezaji msimu huu kwa kumnunua mchezaji mkali wa soka Radamel Falcao.
Man United imempata mchezaji huyo kwa kipindi kizima cha msimu huu kwa mkopo.
Falcao ambaye lazima apitie ukaguzi wa kimatibabu alihusishwa na mpango wa kuihama klabu ya Monaco ambako alisajiliwa kwa kima cha dola milioni hamsini mwaka 2013.
Baadhi waliona taarifa hizo kama fununu tu.
Bila shaka usajili wa Falcao katika Manchester United unaonekana kama mapinduzi kwani vilabu vingi vilikuwa vimemuotea Falcao ambaye anachezea klabu ya Ufaransa ya Monaco.
Falcao ameingiza mabao 11 na kucheza katika mechi 20 za Monaco. Mkataba huo unaipa fursa Manchester United kumnunua mchezaji huyo kwa pauni milioni 43.5 mwishoni wa kipindi cha mkopo.
Klabu ya Louis van Gaal ambayo kama vilabu vingine Ulaya vilifajhamu tu kumhusu mchezaji huyo na uwezo wa kununua katika dakika za mwisho mwisho.
Wakati huohuo, Manchester United itaikopesha Real Madrid mchezaji wake nyota Javier Hernandez.

Brendan Rodgers amfagilia Super Mario Balotelli

Rodgers: Super Mario Balotelli Anastahili Pongezi (Video)
Meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amempa tano mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Super Mario Balotelli kufuatia uwezo safi aliouonyesha wakati wa mchezo wa ugenini dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Rodgers ambaye alikishuhudia kikosi chake kikicheza mchezo wa 100 tangu alipoanza kazi huko Anfield miaka miwili iliyopita amesema kwa hakika Balotelli alionyesha soka safi na anaamini ilikuwa tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa na mashabiki wengi.
Amesema mara nyingi huwa ni vigumu kwa mchezaji yoyote kucheza vizuri katika mchezo wa kwanza hasa ikizingatiwa Balotelli alimsajili mwanzoni mwa juma lililopita akitokea nyumbani kwao Italia alipokuwa akiitumikia klabu ya AC Milan.
cheki alichokisema hapo chini;