
Meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amempa tano
mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Super Mario Balotelli kufuatia uwezo safi
aliouonyesha wakati wa mchezo wa ugenini dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Rodgers ambaye alikishuhudia kikosi chake kikicheza mchezo wa
100 tangu alipoanza kazi huko Anfield miaka miwili iliyopita amesema kwa hakika
Balotelli alionyesha soka safi na anaamini ilikuwa tofauti na ilivyokuwa
inatarajiwa na mashabiki wengi.
Amesema mara nyingi huwa ni vigumu kwa mchezaji yoyote kucheza
vizuri katika mchezo wa kwanza hasa ikizingatiwa Balotelli alimsajili mwanzoni
mwa juma lililopita akitokea nyumbani kwao Italia alipokuwa akiitumikia klabu
ya AC Milan.
cheki alichokisema hapo chini;
No comments:
Post a Comment