
Leo ni siku ya mwisho ya kusajili wachezaji wapya katika vilabu vya soka nchini Uingereza.
Klabu ya Manchester
United ndio inalenga kuweka kufuli kwenye dirisha la usajili wa wachezaji msimu
huu kwa kumnunua mchezaji mkali wa soka Radamel Falcao.
Man United imempata
mchezaji huyo kwa kipindi kizima cha msimu huu kwa mkopo.
Falcao ambaye lazima
apitie ukaguzi wa kimatibabu alihusishwa na mpango wa kuihama klabu ya Monaco
ambako alisajiliwa kwa kima cha dola milioni hamsini mwaka 2013.
Baadhi waliona taarifa
hizo kama fununu tu.
Bila shaka usajili wa
Falcao katika Manchester United unaonekana kama mapinduzi kwani vilabu vingi vilikuwa
vimemuotea Falcao ambaye anachezea klabu ya Ufaransa ya Monaco.
Falcao ameingiza mabao 11
na kucheza katika mechi 20 za Monaco. Mkataba huo unaipa fursa Manchester
United kumnunua mchezaji huyo kwa pauni milioni 43.5 mwishoni wa kipindi cha
mkopo.
Klabu ya Louis van Gaal
ambayo kama vilabu vingine Ulaya vilifajhamu tu kumhusu mchezaji huyo na uwezo
wa kununua katika dakika za mwisho mwisho.
Wakati huohuo, Manchester
United itaikopesha Real Madrid mchezaji wake nyota Javier Hernandez.
No comments:
Post a Comment