MKAZI
wa Kijiji cha Bwekela wilayani Igunga mkoani Tabora, Kashinje Shima, anatafutwa
na Uongozi wa kijiji hicho, kwa kumpa ujauzito mwanawe wa kumzaa mwenye umri wa
miaka 17.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Bwekela, ambaye pia ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya
Igoweko, Robert Ruhende, alilaani kitendo kilichofanywa na mzazi wa mtoto huyo
na kusisitiza kuwa
sheria lazima ichukue mkondo wake.
Akisimulia
kisa hicho, mke wa mkazi huyo ambaye pia ndiye mama mzazi wa mtoto huyo, Geni
Njiro, alidai alibaini hali hiyo Julai 23 mwaka huu, baada ya mwanawe wa kiume
kumfumania baba
yake
na dada yake.
Kwa
sasa kwa mujibu wa Geni, mwanawe huyo ambaye inadaiwa amekiri kushiriki kitendo
hicho, ana ujauzito wa miezi saba.
Geni
alidai kabla ya kugundua kitendo hicho cha kinyama kilichokuwa kikifanywa na
mumewe, alihisi kuwa baba wa mtoto huyo alikuwa akitumia mwanya wa yeye mama
kutokuwepo nyumbani,
kufanya
vitu visivyo vya kawaida.
Alidai
kuwa alipata hofu kuhusu mwenendo wa mumewe na mtoto wake siku moja walipokuwa
shambani wakiendelea na shughuli za kuvuna mazao, ambapo mumewe aliaga kurudi
nyumbani.
Kutokana
na hofu hiyo, Geni alidai aliamua
kumtuma mtoto wake mkubwa wa kiume, ambaye hakutaka kumtaja jina, akafuatilie
nyumbani kupata uhakika wa kile alichokuwa akihofia.
Mama
huyo alidai baada ya mtoto wake huyo kufika nyumbani, ndipo alikuta baba yake
wakifanya ngono na mdogo wake na kurudi shambani na kumpa taarifa mama yake.
Baada
ya taarifa hiyo, mama huyo alidai kuwa aliamua kuita ndugu wa pande zote mbili,
kwa ajili ya kuzungumzia unyama huo, ambapo baba huyo alipohojiwa katika kikao
hicho cha familia,
alikana kuhusika na tuhuma hizo.
Hata
hivyo, mama huyo alidai babu wa mtoto huyo, alishauri waende kupima hospitali
kupata ukweli, ndipo baba huyo alipokubali kuwa anatembea na mtoto wake.
Baada
ya kukubali, inadaiwa baba huyo alitakiwa kulipa adhabu ya faini ya ng’ombe
wawili, ambao aliwalipa na suala hilo kuwa limekwisha. Mwenyekiti wa Kitongoji
cha Mwina, Bundala
Makelema,
alikiri kuwepo kwa suala hilo.
Alidai
kuwa wakati mtuhumiwa huyo akilipa adhabu ya kimila ya ng’ombe wawili, yeye
alishiriki kwa nafasi yake ya Kiongozi wa Kitongoji.
Hata
hivyo, inadaiwa familia anayotoka mama huyo, ilipinga uamuzi huo wa kifamilia
na kumruhusu ndugu yao, kuchukua hatua zaidi, ikiwemo kutoa taarifa katika
vyombo vya habari.
Taarifa
hiyo ilipofika kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bwekela, ambaye pia ni Kaimu
Ofisa Mtendaji wa
Kata
ya Igoweko, Ruhende ambaye aliahidi kwenda Polisi ili hatua zaidi zichukuliwe,
mama huyo alidai ndipo mumewe alipoamua kutoroka nyumbani na kwenda
kusikojulikana.
Source:Habari Leo
No comments:
Post a Comment