Nay
wa Mitego anatarajia kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Nimewaka’ ambapo pia
ametoa sababu ya kuachia nyimbo mfululizo.
Nay
akiwasili Mwanza kwenye Fiesta
Nay
ambaye aliachia wimbo wa Mr Nay hivi karibuni amesema kuwa inambidi aachie
wimbo mpya ili kuwapa mashabiki muziki
ambao adai wanaupenda.
“Kiukweli
kabisa mimi nina mashabiki wengi na wa aina nyingi, kuna mashabiki ambao
wanapenda nikiwa nafanya Hip Hop pia nina mashabiki ambao wanapenda mimi
nikiimba na bahati nzuri ninashukuru nimeanza ku-maintain sehemu zote mbili.
Nikienda kwenye kuimba nafanya vizuri
zaidi,
nikija kwenye kurap nafanya vizuri zaidi pia na nimeshatoa ngoma ya Mr Nay nayo
inafanya vizuri kupita maelezo, kitu ambacho sikuwa na uhakika kama utafanya
vizuri kwa sababu huwezi kujua muziki watu wanaupokea vipi. Lakini namshukuru
mwenyezi Mungu nashukuru mashabiki
wangu, media pamoja na wadau wote,” amesema
Nay.
“Pia
huu ni wakati kwa watu wangu wa mchaka mchaka
narudi tena kwenye ngoma za biashara ninaweza kusema. Inaitwa ‘Nimewaka’
nimewaka nikashasema nimewaka wale watu wangu wanajua namaanisha nini. Huu ni muda
wa kuondoa stress na kutuliza moyo na kutumia ulichonacho iwe ni
bar
iwe mtaani iwe ni wapi. Video ya Mr Nay inatoka panapo majaliwa soonas possible
Jumatatu au Jumatano video itakuwa tayari. Nafikiri nikipata nafasi ndani ya
weekend ijayo nitakimbia kwenda kushoot video ya wimbo ‘Nimewaka’. Nafikiri ni
wimbo ambao utaachana muda mchache sana
kati ya audio na video. Ikitoka audio leo
nafikiri video inaweza ikatoka wiki inayofuata. Video ya Nimewaka ninaweza
nikachukua watu toka Kenya na tukafanyia hapa ndani ama nikaenda Dubai au USA
bado nipo kwenye maandalizi ya mwisho.
No comments:
Post a Comment