
Kuwasili nchini kwa kocha raia wa Zambia
klabuni, Simba SC siku ya jana ni kama kume ‘ wachengua’ mashabiki wengi wa
timu hiyo. Kocha huyo hataki kuonekana kama ‘ kiraka wa muda’ na anataka kuwa
katika mipango ya muda mrefu ambayo itakuwa na mafanikio. ” Nimerudi tena Simba
kurejesha heshima na mafanikio yaliyopotea” alisema, Phiri kocha ambaye
aliipatia timu hiyo ubingwa bila kupoteza mchezo wowote msimu wa 2009/10.
Phiri anakuwa mwalimu
wa tano sita kufanya kazi klabuni hapo tangu, Mei, 2011, Milovan Curkovic pekee
alifanikiwa kushinda ubingwa wa Bara msimu wa 2011/12 msimu ambao Simba
ilifundishwa na makocha wawili baada ya kufutwa kazi kwa Mganda, Moses Basena
baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza. Akiwa na matarajio makubwa ya
kupata ushirikiano kutoka kwa wachezaji, viongozi na mashabiki, Phiri ametoa
ahadi ya kuurejesha ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Patrick Phiri akisaini mkataba wa mwaka mmoja
leo hii mbele ya rais wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na mjumbe wa kamati
ya utendaji Colin Fritch,anayeshuhudia ni meneja wa Phiri ambaye pia ni mtoto
wake, Melesiana Phiri.
” Nitaipa Simba ubingwa wa ligi kuu msimu
ujao” alisema maneno hayo kwa kujiamini licha ya kutambua kuwa timu nyingine
zimejiandaa vya kutosha huku makocha kama, Patrick Omog wa Azam FC na Marcio
Maximo wa Yanga SC wakinoa na kuwekeza mbinu na ufundi katika vikosi vyao kwa
zaidi ya mwezi mmoja sasa. Mashabiki wa Simba wamefurahi kuona mwalimu huyo
aliyewapa ubingwa mwaka 2004 akirejea na hivyo pia kwa Phiri ambaye ameushukuru
uongozi wa klabu hiyo kumuamini na kumrejesha Tanzania sehemu anayosema ni ‘
nyumbani kwake kwa pili baada ya nchi yake ya Zambia’
. ” Tanzania ni nyumbani kwangu, nafurahi
kurudi kufanya kazi katika nchi hii ambayo naichukulia kama nchi yangu ya pili
“.
Phiri alizungumza maneno hayo mara tu baada ya
kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu hiyo yenye maskani kwenye mitaa
ya msimbazi jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment