Friday, August 8, 2014

MKWARA WA LOGARUSIC WAONGEZA MORALI YA CASILASS SIMBA SC


Kipa wa Simba, Hussen Sharrif 'Casillas'
KOCHA wa Makipa wa Simba, Iddi Pazi, amesema kitendo cha kocha mkuu wa timu hiyo, Zdravko Logarusic kuonyesha kutokumkubali kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ aliyesajiliwa kikosini hapo kutokana na kuwa na mwili mdogo, kimepandisha morali ya kipa huyo na ameapa kumshawishi kocha huyo kwa njia zote ili ampatie nafasi kikosini hapo.
Logarusic alipendekeza klabu hiyo isajili kipa mwenye uwezo wa juu na mwenye mwili mkubwa, lakini Kamati ya Usajili ya klabu hiyo iliposhindwa kumpata kipa mwenye vigezo hivyo viwili, iliamua kumsajili Casillas ambaye ndiye alikuwa kipa bora msimu uliopita alipoichezea Mtibwa Sugar.
“Bado naendelea na programu yangu ya kumpatia mazoezi makali, maneno ya kocha yalionekana kumkatisha tamaa mwanzoni, lakini kwa sasa morali yake iko juu, ameapa kumwonyesha kocha Logarusic kuwa umbo si kitu,” alisema Pazi.
“Kwa siku chache nilizomfanyisha programu yangu hiyo, ameonekana kuipenda, ameanza kunipa moyo kuwa kwa siku zijazo ataweza kumshawishi kocha akasahau kabisa kuhusu udogo wa umbo lake.”
                                      Source:Mwanaspoti

No comments:

Post a Comment