
NYOTA mpya wa Real
Madrid, James Rodriguez amesema kushinda kiatu cha dhahabu katika fainali
za kombe la dunia ilikuwa ndoto iliyotimia.
Mshambuliaji huyo
mwenye miaka 23 aliposti picha katika mtandao wa Twita akiwa na tuzo ya kiatu
cha dhahabu aliyoshinda baada ya kufunga mabao sita katika fainali za kombe la
dunia majira ya kiangazi nchini Brazil.
Ili kushangilia tuzo
hiyo, nyota huyo wa Colombia atacheza msimu ujao kwa kutumia viatu vya dhahabu
na anatarajia kuongeza mabao mengi zaidi.
"Nilikuwa na matumaini
ya kushinda kwasababu mara zote nilikuwa naota kushinda kitu kama hiki,' James
aliwaambia waandishi. 'Hii pia ni chanzo cha furaha kwa nchi yangu ya Colombia.
Kwasababu walinipa nguvu sana, kwahiyo nilitakiwa kushinda tuzo.'
Viatu vipya: Kiungo huyu wa Colombia atachezea viatu vya dhahabu msimu ujao kama sehemu ya kusherehekea mafanikio.
MABAO YA RODRIGUEZ KOMBE LA DUNIA 2014
· Alifunga moja, na
kutengeneza moja dhidi ya Ugiriki.
· Alifunga moja, na
kutengeneza moja dhidi ya Cameroon ·
Alifunga bao zuri
dhidi ya Japan
·
·
Alifunga mabao mawili
dhidi ya Uruguay, likiwemo bao la mashindano
·
·
Alifunga penati
Colombia wakifungwa 2-1 na Brazil katika mchezo wa robo fainali.
No comments:
Post a Comment