
Kocha Patrick Phiri
Mazungumzo
yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa baina ya Patrick Phiri kutoka Zambia
(pichani) na Simba SC na sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi, akisaidiwa na
Nahodha wake enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah Matola’Osama’
Phiri
ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa
makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa
ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi
moja.
Lakini
pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni
jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.
Katika
awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani
amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.
Kwa
sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na
Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya
Zambia.
Phiri
ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United
(sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji,
Alikuwemo
kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya
Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya
mwaka 2008 nchini Ghana
Akiwa
kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20
ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria
mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka
1999
Simba
SC imevunja mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada
ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki
juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Loga
ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa
kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu.
Rais
wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema jana kwamba uamuzi huo umekuja baada ya
kumvumilia kwa kiasi cha kutosha
Loga
ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana,
kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane
Loga
aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif aliikuta Simba SC bado
ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya
nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.
No comments:
Post a Comment