Jeshi
la Polisi Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, linamtafuta mkazi wa malangali,
Bw.Simon Paskali kwa kosa la kuwapiga watoto wa, kumuua mmoja na kukimbia
pasikojulikana.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia jana babaada ya mtuhumiwa kurudi nyumbani
akitokea kwenye sherehe ya komunio akiwa amelewa na kuanza kuwapiga watoto wake
kwa fimbo hadi wakazirai.
Akizungumzia
Tukio hilo , Kaimu kamanda wa wa polisi
mkoani Humo, Frednand Rwegasila, alisema mtuhumiwa alikuwa akiishi na
watoto muda mrefu baada ya kuachana na mkewe.
Aliwataja
watoto hao kuwa ni Daniel Paskali(11) ambaye ndiye aliyefariki na Jackson
Paskali(9) ambao baada ya kuzirai kwa kipigo na mtuhumiwa kukimbia, majirani
walikwenda kutoa msaadawa kuwapeleka hosptali.
“Wakiwa
njiani, Daniel alifarikidunia wakati Jackson amelazwa katika Hospitali ya mkoa akiendea
kkupatiwa matibabu na ameumizwa sehemu mbalimbali za mwili wake.”Alisema
Kamanda
Rwegasila alisema jeshi hilo linaendelea kumsaka mtuhumiwa ali aweze kufikishwa
mahakamani
No comments:
Post a Comment