Thursday, July 31, 2014
RAIS MUGABE AMTEUA MKEWE KUONGOZA TAWI LA CHAMA CHAKE
Uteuzi usiotarajiwa wa mke wa rais Robert Mugabe kuongoza tawi la chama hicho la wanawake limezusha uvumi mpya kuhusiana na nani atarithi nafasi ya rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90. Uthibitisho wa wadhifa wake kuwa kiongozi wa tawi la umoja wa wanawake katika chama cha ZANU-PF katika mkutano wa kitaifa wa chama mwezi Desemba utamuingiza Grace Mugabe , mwenye umri wa miaka 49 , katika kamati kuu ya chama tawala yenye mamlaka makubwa. Akiwa mjumbe wa chombo hicho chenye nguvu katibu muhtasi huyo wa zamani wa rais atachukua nafasi muhimu katika mapambano ya kumrithi mume wake , ambaye ameingia madarakani mwaka 1980 baada ya zimbabwe kupata uhuru kutoka Uingereza. Mugabe anatimiza mwaka mmoja leo tangu kuingia madarakani baada ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi mwaka jana , ambao umekiondoa chama cha MDC katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment