SIKU
moja baada ya Serikali kuifungia kwa muda usiojulikana Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na
Teknolojia (IMTU), kinachohusishwa na utupaji wa viungo vya binadamu mithili ya
takataka, Serikali mkoani Rukwa nayo imekifungia chuo kingine cha Rukwa College
of Health and Allied Sciences.
Moja
ya sababu ya kukifungia chuo hicho ni kutokuwa na kibali cha Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii huku mitaala ya kozi zake ikiwa haipo, kwa maana ya kupitwa na
wakati.
Kutokana
na kasoro hizo, Serikali ya mkoa kupitia Idara yake ya Afya imezuia wanafunzi
wa chuo hicho kufanya mazoezi ya vitendo katika
Hospitali
ya Mkoa na nyingine mkoani hapa.Chuo hicho kinachomilikiwa na Umoja wa
Kuendeleza Wanawake Mkoani Rukwa (RWAA) ambacho kipo Kanondo, nje kidogo ya Mji
wa Sumbawanga, kwa
sasa
wanafunzi wake wa mwaka wa mwisho wako katika maandalizi ya mitihani yao ya
kuhitimu masomo.
Mitihani
hiyo inatarajia kuanzia Agosti 25, mwaka huu.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk
John Gurisha amelithibitishia gazeti hili juu ya uamuzi huo wa serikali ya mkoa
kwa kile alichosema chuo hicho
kinaendeshwa kinyemela, ikiwa ni kinyume cha utaratibu kwani hata mitaala ya
kozi zinazofundishwa haipo katika mfumo wa masomo Tanzania, hivyo si rahisi
kupata viwango vya ubora wa wanafunzi.
Akifafanua,
Dk Gurisha alisema usajili wa muda uliotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa
(NECTA) haukipi chuo hicho uhalali wa kutoa mafunzo ya tiba, bali kinatoa ruhusa ya kufungua chuo
ili kiweze kutoa kozi za tiba.
Alisema
baada ya kupata usajili huo, chuo kilitakiwa kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii na si vinginevyo.
Aliongeza
kuwa chuo hicho hakifuati mitaala ya Wizara ya Afya kwa kuwa kozi ya wahudumu wa afya inayotolewa
chuoni hapo ilishasitishwa na wizara husika.
“Awali
kabla Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kusitisha kozi ya wahudumu wa afya
ilikuwa ikitolewa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa pekee kwa mantiki hii kozi zinazofundishwa
chuoni hapo ni batili, pia hakina baraka za Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
ambaye ndiye pekee mwenye mamlaka ya
kutoa vibali vinavyowezesha vyuo vya afya kufundisha kozi
mbalimbali.“Hivyo
chuo hiki akitambuliwi, nimezuia pia wanafunzi wa chuo hicho
kufanya
mazoezi ya vitendo katika hospitali hii ya mkoa na zinginezo zilizopo mkoani hapa; sasa kutokana na hili
chuo hicho kinawapeleka wanafunzi wake
Mpanda mkoani Katavi kwa mafunzo ya mazoezi kwa vitendo
….
Niwe wazi wanaosoma katika chuo hicho wanajipotezea muda wao,“
alisema.Aliongeza
kuwa atahakikisha chuo hicho kinafuata utaratibu ili kiweze
kutambuliwa na kwamba haogopi licha ya kauli
kali zinazomshutumu kuwa yeye (Dk
Gurisha) anakipiga vita kwa kuwa si mzawa wa mkoa huo.
“Huwezi
kuchezea maisha na afya za watu kwa sura ya uzawa … kwanza
kama
kweli kingekuwa ni halali ilikuwa ni jambo jema kwetu kwa kuwa baadhi ya
wahitimu wake wangeweza kuajiriwa hospitalini hapa na kwingineko ili kupunguza
upungufu wa wahudumu wa afya wenye ujuzi,“ anaeleza.
Naye
Katibu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, Dorice Nzingilwa anasema wanafunzi wa chuo hicho wanasoma kwa miezi
mitatu kisha wanapelekwa kufanya mazoezi ya vitendo na kuanza kuwatibu
wagonjwa, jambo ambalo linahatarisha maisha ya wagonjwa.
Aidha
alisema hata walimu wanaofundisha katika chuo hicho hawana sifa kwa kuwa baadhi
yao ni matabibu wasaidizi.
Kwa
mujibu wa barua ya Agosti 20, 2013 iliyosainiwa na Dk Gurisha kwenda kwa Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye kumbukumbu namba GHS /T 40/15/4, licha ya
kuainisha mapungufu lukuki
yanachokikabili
chuo hicho pia kimebainisha kuwa kinaendeshwa kinyume cha utaratibu kwa vile
hata mitaala ya kozi zinazofundishwa haipo.
“Hivyo
si rahisi kupata viwango na ubora wa wanafunzi,“ inaeleza sehemu ya barua hiyo. Pia imebainisha kuwa Kaimu
Mkuu wa Chuo hicho ni
Ofisa
Tabibu mstaafu na wengine watatu ambao ni walimu wa kudumu ni wauguzi wastaafu
huku mwingine cheo chake pia makazi yake halali hayafahamiki.
Pia
kwa mujibu wa barua hiyo walimu wa muda ambao ni watano hawafai kufundisha
kwani mmoja wao ni muuguzi mstaafu, wengine tabibu wasaidizi watatu na daktari mmoja kutoka Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Rukwa.
“Timu ya usimamizi wa huduma za afya Mkoa RHMT
na ile ya wilaya CHMT tunapendekeza
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iwe inafanya ukaguzi wa vyuo vinavyotaka
kuanzishwa kabla ya Nacte ili wajiridhishe; na wakati wa kufanya ukaguzi washirikishe timu ya mkoa
na wilaya ili kuondoa au kuepuka migongano isiyo ya lazima kati ya Wizara ya
Afya na Nacte wataarifiwe kwa ajili ya
kukamilisha usajili.
Aidha
Nacte wafahamishwe kwamba wanapotoa usajili msimamizi mkuu na mtoa mitaala ni
Wizara husika … “Na ukaguzi wanaoufanya Nacte uzingatie vigezo vilivyopo kwani hatutegemei kama Rukwa
College of Health Sciences wangepewa
namba ya usajili kwa hali tuliyoikuta wakati wa ziara yetu,” inaeleza sehemu ya
barua hiyo.
Akizungumzia
hayo, Mwenyekiti wa Asasi hiyo ya RWAA inayomikili chuo hicho, Annastela Malaji
anasititiza kuwa chuo hicho ni halali kwa kuwa kimepata usajili wa muda kutoka
Nacte uliotolewa Januari 31,2014 na kitakoma Januari 30,2015 ambapo kilishaanza
kuchukua wanafunzi tangu mwaka jana.
“Tuko
kihalali isitoshe tuna usajili wa Nacte kama kweli tungekuwa hatuna uhalali mbona Agosti 25 mwaka huu
wanafunzi watafanya mitihani yao ya kuhitimu tena wataifanyi katika hospitali
ya mkoa kwa maelekezo ya Wizara husika …. Lipo jambo hapa,“ alisema
Malaji.</p>
Wasifu kufungiwa
IMTU
Katika
hatua nyingine, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kimepongeza uamuzi wa
Serikali wa kuifungia Hospitali ya Chuo cha Kimataifa cha Matibabu na
Teknolojia (IMTU) na kuiomba kufanya ukaguzi kwa hospitali nyingine nchini za serikali na
binafsi.
Hayo
yamesema na Rais wa MAT, Dk Primus Saidia aliyeongeza kuwa, hatua ya serikali
inalinda watu wake na kuhakikisha watoa huduma wanakuwa na sifa stahili, huku wakitoa huduma
bora. Alisema kutokana na taaluma ya afya kuingiliwa na matatizo mbalimbali,
ikiwemo kuwepo kwa watoa huduma wasio na sifa huku wengine wakiwa hawana vifa vya kutosha hivyo ukaguzi
uendele na hospitali nyingine.
Source:HabariLeo
No comments:
Post a Comment