Maajabu
yanaendelea duaniani, wiki hii tuliandika habari kutoka China iliyohusu kijana
aliyeng’olewa meno 132, lakini pia kuna habari nyingine kutoka nchini humo
ambayo imewaacha wengi midogo wazi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shagalist, mwanaume
aliyetajwa kwa jina la Mr. Chen, mwanandoa mwenye umri wa miaka 44 na mkaazi wa
Zhejiang, China amegundulika kuwa alikuwa katika siku zake kama inavyokuwa kwa
wanawake kwa mzunguko wa hedhi(period) baada ya kufika hospitali
akilalamika sana kuwa na maumivu ya tumbo.
Taarifa zilizotolewa na madaktari wa
hospitali ya Yongkang zinaeleza kuwa mwanaume huyo alifanyiwa uchunguzi na
kugundulika kuwa alikuwa na mfumo wa uzazi wa mbegu za mwanamke ingawa alikuwa
na uume.
Ingawa mwanamme huyo aliwaeleza madatari kuwa
amekuwa akishiriki na mkewe tendo la ndoa kwa miaka kumi ya ndoa yao bila
tatizo, madaktari hao waligundua kuwa alikuwa anatoa mkojo wenye damu ambao
uliwasababisha wafanye uchunguzi wa kina na kugundua hali hiyo.
Msemaji wa hospitali hiyo alieleza kuwa
vipimo vya ACT Scan vilionesha wazi kuwa alikuwa na uterus na ovaries (mayai ya
uzazi), na kwamba madaktari walieleza kuwa alikuwa amechelewa kupata matibabu
kwa tatizo lake hilo lisilo la kawaida.
Mr. Chen mwenyewe alieleza kuwa alikuwa
anasikia dalili ya vitu vingi visivyo vya kawadia hata katika maumbile yake, na
kibaya zaidi ni pale alipoanza kuona anatoa damu badala ya haja ndogo.
No comments:
Post a Comment