Sunday, May 18, 2014

JE UNATAKA KUFANIKIWA MAISHANI? SOMA HAPA



Katika mapambani kwenye maisha watu wengi huwa  wanajiuliza maswali mengi, mojawapo ni kwa nini sifanikiwi? Kwa nini mimi tuu? Na wewe unaweza kuwa ni mmoja wao.Leo nataka nikufahamishe jinsi ya kufanikiwa maishani na kubadili kabisa maisha yako.Zifuatazo ni njia zitakazo kuwezesha wewekufanikiwa maishani.
1.Acha kulaumu wengine na kujitetea.
Haijalishi kama tatizo linalokukabili limesababishwa na nani, ama wewe au mtu mwingine cha msingi ni kupata ufumbuzi wa tatizo.Wengi wetu tatizo likitoke huwa tunakimbilia kuwalaumu wengine na kujitetea kwa njia hii hautaweza kufanikiwa maishani. Elewa kwamba umebeba dhamana ya maisha yako mwenyewe na hakuna mtu yeyote wa kubadilisha maisha yako ila wewe mwenyewe.
Pale tatizo linapotokea kitu cha kwanza na cha msingi ni kutafuta chanzo cha chake na kuanza kulitatatua mara moja.
2.Acha kusitasita/Acha tabia ya kuahirisha mambo.
Unapokuwa unataka kufanya kitu, usiwe na tabia ya kuahirisha bila sababu ya msingi.Kwa kufanya hivi hutafanikiwa kwa sababu mambo yako uta kuwa unayafanya kwa maneno kuliko vitendo.
Ukitaka kufanikiwa maishani usiwe na tabia ya kuahirisha kila kitu kwamba ntafanya kesho, kumbuka kesho huwa haifiki daima! Jitahidi kufanya mambo yako muda huohuo.Tambua kwamba matendo ndo kila kitu katika maisha.
3.Tambua na Kuza kipaji chako.
Utafiti unaonyesha kuwa watu wengi hawajafanikiwa katika maisha kwa sababu wanafanya kazi zisizoendana na ujuzi wao.Kitu kikubwa katika maisha ni kutambua ujuzi wako.kila mtu duniani ameumbwa na kipaji  fulani ama anao uwezo wa kufanya shughuli fulani vizuri zaidi yaani kwa urahisi kuliko nyingine. Ukitambua shughuli unayoweza kiuifanya kwa urahisi kuliko nyingine na hata saa nyingine unaweza kushangaa uliijifunza vipi, tambua hicho ndicho kipaji chako na fanya kila linalowezekana kukikuza na kukiendeleza.
4.Kuwa na malengo.
Kuweka malengo na mikakati ya kutimiza hayo malengo ni jambo kubwa na la msingi katika maisha.Watu wengi huwa wanaweka malengo bila kuweka mikakati ya kuyafikia malengo yao.Kwa kufanya hivi ni sawa na kijidanganya.
Kinachotakiwa ili ufanikiwa lazima uweke malengo na mikakati ya kufikia malengo hayo. kuweka malengo kunahitaji kujipa muda pia wa kuyatimiza malengo hayo.Ili kufikia malengo yako kirahisi unatkiwa kuwaza kama vile una muda mfupi wa kuwa hapa duniani  
Kwa maoni au ushauri tuma; bongoleotz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment