
KOCHA
mpya wa Simba, Patrick Phiri ametua jana Dar es Salaam na kuahidi kurudisha
heshima ya Simba.
Kocha
huyo raia wa Zambia, alitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), saa 7:30 mchana na kupokewa na wajumbe watatu wa Kamati ya
Utendaji, Said Tully, Collin Frisch na Idd Kajuna pamoja na baadhi ya mashabiki
waliokuja kumlaki.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kutoka nje ya uwanja huo, Phiri alisema
anamshukuru Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva kwa kumpa kazi na kuahidi
kurudisha ubingwa.
“Tanzania
ni nyumbani kwangu kwa pili, nashukuru kurudi tena katika klabu hii,
nitajitahidi kufanya kazi kwa bidii na kuleta heshima,” alisema Phiri.
Mzambia
huyo aliyewahi kuinoa Simba kwa vipindi viwili tofauti, anakuja kurithi mikoba
ya Zdravko Logarusic, raia wa Croatia, aliyefukuzwa Jumapili.
Phiri
alisema alikuwa akiifuatilia timu kwa muda mrefu kwani imekuwa na matatizo,
lakini sasa, baada ya kurudi anaamini mambo yatakuwa mazuri msimu ujao.
“Simba
ilikuwa ina matatizo kwa muda mrefu, nitayaondoa kwa sababu naijua klabu hii
vizuri,” alisema na kuwashukuru mashabiki na wote waliofika kumpokea kwenye
uwanja huo wa ndege.
Hata
hivyo, chanzo kimoja cha Simba kilisema kuwa huenda akasaini mkataba wa miaka
miwili. Kuja kwake katika klabu hiyo ni kwa mara ya tatu, ikiwa alikuja kwa
mara ya kwanza msimu wa 2003 hadi 2005 na baadaye mwaka 2006 hadi 2008.
Phiri
aliiongoza Simba kunyakua ubingwa na kumaliza msimu wa mwisho bila kupoteza
mechi hata moja.
Tafadhali like page yetu kwa habari motomoto zaidi
ReplyDelete