Thursday, August 14, 2014

Afande Sele azungumia kifo cha Mama Tunda, adai ni uzembe wa madaktari

Rapper wa Morogoro Afande Sele amesema kifo cha aliyekuwa mke wake, Mama Tunda kimetokana na uzembe wa madaktari. Mama Tunda amefariki baada ya kulazwa kutokana na kuugua Malaria.
Afande Sele akiwa na mzazi mwenzake Mama Tunda enzi za uhai wake
Akizungumza na Bongo5 leo, Afande amedai kuwa bila uzembe wa madaktari huenda malaria isingechukuauhai wa Mama Tunda.
“Mama Tunda ametuachia pengo kubwa sana kwenye familia,” amesema Afande. “Amefariki jana saa tano usiku katika hospitali kubwa hapa Morogoro kutokana na uzembe wa madaktari. Walimpa matibabu akarudi nyumbani, sitaki kulizungumzia kiundani kwa sasa hivi kwa sababu tupo kwenye wakati mgumu. Huku mazishi yatafanyika kuanzia kama saa tisa hivi lakini bado hatutajua itakuwa wapi bado tupokwenye mipango. Malaria ilimchukua sana, kwa familia na watoto kwetu ni msiba mkubwa sana, yaani ni huzuni sana,” ameongeza Afande.
 source:Bongo5

No comments:

Post a Comment