Shilole
si mgeni katika kuota vitu vikubwa. Kutoka kwenye ndoto yake ya kufanya kolabo
na Jennifer Lopez, awamu hii ameenda
mbali zaidi. Muimbaji huyo amechoka ‘Kuchuna Mabuzi’ na sasa anataka kuingia
mjengoni. Mrembo huyo ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohamed, amepanga
kugombea ubunge kwenye jimbo analotokea la Igunga mkoani Tabora katika uchaguzi
wa mwaka 2015!
Akizungumza
kwenye kipindi na Sizi Kitaa cha Clouds TV, Shilole amesema yupo serious na nia
hiyo na kama Mungu akipenda atakuwa mbunge wa jimbo hilo.
“Baada
ya Dokta Dalali Kafumu anayefuata ni mimi,” amesema Shilole. “Mimi nadhani
napenda jimbo langu na napenda wakazi wangu wa Igunga wananiona toka nakua
mpaka sasa hivi, kwahiyo wanafurahi. Sasa wananiambia ‘sisi hatutaki kumpa mtu
mwingine kiti hiki sasa wananipa changamoto. Vitu viwili vya kwanza ambavyo
nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza
nitatetea haki za wasanii, cha pili
Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani akina mama, wale
mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo nitawatafutia kazi,
nitajenga chuo cha muziki,” alijinadi muimbaji huyo.
“Mimi
jimbo langu nalijua na nimekua pale mpaka nimekuwa mkubwa lazima nilitimize
sitaki wananchi wangu wapate tabu. Mimi nadhani wanaoenda kugombea majimbo
yasiyo ya kwao wanaweza fanya chochote, lakini kama ni wa hapo lazima itakuuma.
Lakini unakuta mtu wa Dar es salaam anakwenda kugombea Mtwara huko nani
anamjua? Mimi nitaenda kugombea kwangu lazima nitapata kura lazima watanipa!
Kwahiyo kaeni tayari Shilole ni mbunge mtarajiwa Igunga,” alitamba

No comments:
Post a Comment