Shirikisho
la soka la Brazil CBF, limemtangaza aliyekuwa mchezaji wa Brazil, Dunga kuwa
kocha wa timu ya taifa kwa mara ya pili.
Dunga
aliyeiongoza Brazil kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1994
aliwahi
pia kuwa kocha katika mwaka wa 2006 hadi 2011. Dunga amechukua
nafasi
ya Luiz Felipe Scolari, ambaye
alijiuzulu kufuatia kimbunga cha
mabao
7-1 ambayo timu hiyo ililazwa na Ujerumani katika hatua ya nusu
fainali
.
Scolari
mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Brazil katika semi fainali
za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata
kichapo kibaya cha mabao
masaba
kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la Dunia Ujerumani.
Dunga
amewapiku mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa
kilabu
ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye
aliwahi
kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
Wachezaji
wanamtaka kocha Sabella kuiongoza timu hiyo katika kipute
cha
kuwania ubingwa wa mataifa ya Amerika ya Kusini yaani 2015 Copa
America
mashindano yatakayoandaliwa huko Chile.
Source:BBC
No comments:
Post a Comment