Thursday, July 31, 2014

RAIS MUGABE AMTEUA MKEWE KUONGOZA TAWI LA CHAMA CHAKE

 
Uteuzi usiotarajiwa wa mke wa rais Robert Mugabe kuongoza tawi la chama hicho la wanawake limezusha uvumi mpya kuhusiana na nani atarithi nafasi ya rais Mugabe mwenye umri wa miaka 90. Uthibitisho wa wadhifa wake kuwa kiongozi wa tawi la umoja wa wanawake katika chama cha ZANU-PF katika mkutano wa kitaifa wa chama mwezi Desemba utamuingiza Grace Mugabe , mwenye umri wa miaka 49 , katika kamati kuu ya chama tawala yenye mamlaka makubwa. Akiwa mjumbe wa chombo hicho chenye nguvu katibu muhtasi huyo wa zamani wa rais atachukua nafasi muhimu katika mapambano ya kumrithi mume wake , ambaye ameingia madarakani mwaka 1980 baada ya zimbabwe kupata uhuru kutoka Uingereza. Mugabe anatimiza mwaka mmoja leo tangu kuingia madarakani baada ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi mwaka jana , ambao umekiondoa chama cha MDC katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Kijiji chafunikwa na maporomoko,India

 
Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katika kijiji cha kijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo huo, japo kuwa mazingira magumu na hali mbaya ya hewa vinakwamisha shughuli hiyo.Maporomoko hayo yaliyokikumba kijiji cha Malin India karibu na jimbo la Maharashtra yamesababisha nyumba nyingi kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia katika eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Devidas Desh pande aliyepo katika eneo la tukio anasema jingo pekee linaloonekana kunusurika na janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.

Kama ulimiss kushuhudia mahojiano ya Diamond na mwandishi wa Habari baada ya Kupewa Tuzo, cheki hapa


Wednesday, July 30, 2014

WATUHUMIWA 10 WA UJAMBAZI WAKAMATWA NA SILAHA NZITO



 
MAJAMBAZI 10 wanaounda mtandao hatari wa uhalifu nchini, wametiwa mbaroni wakati wa msako mkali uliofanikisha pia kukamatwa kwa silaha mbalimbali.
Silaha hizo ni bunduki tisa zikiwemo SMG tatu, bastola mbili, short gun nne na risasi 15 zilikamatwa.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliyasema hayo ofisini kwake kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.
Katika msako huo watuhumiwa walisachiwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 9 kama ifuatavyo:-
SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670 Na risasi 6  ndani
S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic
SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako
Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:
1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala Charambe.
2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara Kibondemaji.
3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
4. SAID S/O FADHIL MLISI – miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Gongolamboto
5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa Gongolamboto
6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo
7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo Kilakala
10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilakala
Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O  YOHANES VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG Katika baadhi ya matukio wananchi walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo
Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo
Hivyo tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.
Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya Mwanasheria wa Serikali kutafuta majalada yao ya kesi mbali mbali
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM