Friday, September 5, 2014

SIFA YA KIDATO CHA NNE KUWA MBUNGE SASA YAPINGWA.



 
KAMATI nyingi za Bunge Maalumu la Katiba, zimekataa sifa ya elimu ya kidato cha nne, kuwa kigezo cha msingi cha mgombea ubunge, kwa madai kuwa inabagua wananchi kwa kuondoa haki yao ya kidemokrasia ya kuomba kupigiwa kura na kupiga kura.
Hata hivyo, kamati hizo zimeweka sifa ya kuwa mbunge, iwe ni kujua kusoma na kuandika, bila kufafanua kama sifa hiyo nayo, inaweza kuleta ubaguzi huo.
Ibara ya 26 kifungu cha kwanza cha rasimu ya Katiba, kinaeleza kuwa sifa ya kugombea ubunge ni kujua kusoma na kuandika, lugha ya Kiswahili na Kiingeza na ana elimu isiyopungua kidato cha nne.
Lakini taarifa za kamati nyingi zimeeleza kuwa suala la kugombea nafasi yoyote ni la kidemokrasia, haipaswi mtu kuzuiwa kugombea kwa kigezo cha elimu, kwani hii ni haki ya kikatiba.
Katiba haitakiwi kuweka kigezo chochote kinachokiuka haki za msingi za kuchaguliwa au kuchagua,” ilisema taarifa namba 10 ya Bunge hilo. Kamati hiyo pia ilisema haki ya kuamua kama mgombea anafaa au hafai ni ya wapiga kura, wasizuiwe kikatiba kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua mtu wanayemtaka.
Walisema utaratibu huo haupo duniani kote hata nchi zilizokomaa na demokrasia iliyokomaa.
Ni kamati namba mbili tu, ndio ambayo imetaka sifa ya mtu kuwa mbunge iwe elimu ya kidato cha nne, lakini pia awe ni raia wa kuzaliwa na hana uraia wa nchi nyingine na aliyetimiza umri wa miaka 21.
Kuhusu watu ambao waliwahi kukutwa na makosa ya jinai kutogombea, baadhi ya kamati zinapendekeza kuwa makosa hayo yawe ya ubakaji au ujangili, ili kutowakataza waliohukumiwa kwa makosa madogo madogo ya jinai na kunyimwa fursa ya kugombea nafasi ya ubunge.
Wajumbe hao pia wametaka ibara ya pili (a) inayozungumzia muda wa ukomo wa ubunge wa vipindi vitatu, ifutwe ili kuwapa fursa wabunge ambao ni watendaji wazuri katika maeneo yao, kuendelea kugombea na kuchaguliwa na wananchi kwa sababu kimsingi ni haki ya mtu kikatiba.
Pia walisema hiyo itawapa uhuru wananchi kuchagua mbunge wanayemtaka, hata kama ameshashika madaraka hayo kwa vipindi vitatu mfululizo.
Hata hivyo wametofautiana katika eneo la watumishi wa umma wanapoamua kugombea ubunge, urais na udiwani makamu wa rais au nafasi nyingine katika chama cha siasa, wapo wanataka mtu huyo utumishi wake ukome pale anapogombea, lakini wapo wanaotaka mtumishi huyo ahesabiwe kama yuko likizo bila malipo.
Kwa upande wa uongozi wa Bunge, karibia kamati zote zimekubaliana na rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ambayo yanataka mbunge, waziri, naibu waziri wasiruhusiwe kugombea uspika wala unaibu uspika.
Sababu za kukubaliana na hoja hiyo ni kwamba ni kutoa uhuru kwa spika na naibu wake kufanya kazi yake kwa uhuru bila kuingiliwa na chama chake cha siasa.

Aliyempiga kichwa mwamuzi aadhibiwa



  
                                              Ismail Gunduz
Mchezaji Ismail Gunduz wa SK Rum ya Austria amefungiwa kuto cheza mechi 70 ikiwa ni adhabu baada ya mchezaji huyo kumpiga kichwa uwanjani mwamuzi wa mchezo.
Gunduz anayechezea timu ya daraja la tano ya SK RUM alimpiga mwamuzi siku ya Jumamosi kwa kichwa muda mfupi kabla ya mwamuzi huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo.
Hata hivyo mwamuzi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kugongwa kichwa hicho.
Kwa mjibu wa sheria za soka za taifa hilo adhabu ya juu kwa kosa kama hilo ni kufungiwa michezo 108.

Wednesday, September 3, 2014

VAN PERSIE:NIKO TAYARI KUPIGANIA NAMBA NA FALCAO

Van Persie: I'm ready to fight Falcao
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie amesema yuko tayari kupigania namba na mchezaji mwenzake Radamel Falcao katika klabu ya Manchester United. Baada ya usajili wa Falcao sasakuna wachezaji kadhaa watakaopigania namba katika klabu hiyo.
Wachezaji watakopigania namba katika klabu hiyo ni Wayne Rooney, Van Persie and Juan Mata.

CHEKI PICHA ZA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA LILIPOTEKETEA KWA MOTO

Name:  big.jpg
Views: 0
Size:  139.7 KB
Name:  big.jpg
Views: 0
Size:  88.4 KBName:  big.jpg
Views: 0
Size:  85.2 KBName:  big.jpg
Views: 0
Size:  30.0 KB

Tuesday, September 2, 2014

HUU NDIO UHAMISHO WA WACHEZAJI KUMI GHALI ZAIDI KUFANYIKA KWENYE DIRISHA HILI LA USAJIRI.

Suarez to Barcelona and the 10 most expensive transfers of the summer
Dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi kwa vilabu majira haya ya kiangazi limefungwa hapo jana usiku tukishuhudia miezi kadhaa ya kufuru ya matumizi yaliyokithili ya pesa kwa vilabu barani Ulaya.

Japokuwa rekodi ya uhamisho ghali zaidi duniani inashikiriwa na Gareth Bale ya uhamisho wa Euro milioni 100 alipohama kutoka Tottenham kwenda Real Madrid mwaka uliopita lakini mado suala la matumizi ya fedha na uvunjwaji wa rekodi mbalimbali linabakia palepale kwa vilabu kadhaa barani Ulaya.
Little bit hefty! United paid a club record £60million for Real Madrid midfielder Angel di Maria 
Wakati vilabu vikiendelea kusharehekea mapato makubwa kwenye matangazo na mauzo ya vifaa mbalimbali isivyo kawaida na vikienda kwenye duka kuu la ununuzi wa wachezaji ambalo ni michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika kule nchini Brazil, Vilabu vinaonekana kuongeza ushindani pia kwenye matumizi ya mapato hayo makubwa wanayojikusanyia kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato.

Ufuatao ni usajili wa wachezaji kumi ambao wamenunuliwa kwa mahela mengi kwenye msimu huu wa manunuzi.
No.MchezajiKutokaKwendaAda (Euro)
1Luis SuarezLiverpoolBarcelona88m
2James RodriguezMonacoReal Madrid80m
3Angel Di MariaReal MadridManchester United75m
4David LuizChelseaParis Saint-Germain49.5m
5Eliaquim MangalaPortoManchester City44.5m
6Diego CostaAtletico MadridChelsea44m
7Alexis SanchezBarcelonaArsenal40m
8Luke ShawSouthamptonManchester United37.8m
9Ander HerreraAthletic BilbaoManchester United36.5m
10Cesc FabregasBarcelonaChelsea36m